Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO na UNICEF zamulika haja ya kuboresha upatikanaji maji na usafi

Mtu anawa mikono Picha ya WHO

WHO na UNICEF zamulika haja ya kuboresha upatikanaji maji na usafi

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Bado hakuna usawa katika upatikanaji wa maji safi ya kunywa na huduma za kujisafi kote duniani, imesema ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani, WHO na lile la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF.

Ripoti hiyo inayohusu maendeleo katika upatikanaji wa maji ya kunywa na huduma za kujisafi, inaonyesha kuwa tangu mwaka 1990, takriban watu bilioni 2 duniani wanapata huduma bora zaidi za kujisafi na maji ya kunywa kutoka vianzo bora zaidi vya maji.

Ripoti hiyo inasema pia kuwa zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani wanaishi mijini, na miji bado ina huduma bora zaidi za maji safi ya kunywa na kujisafi kuliko wale waishio vijijini.

Ripoti inasema watu wapatao bilioni 1.6 wanapata maji kwa njia ya mabwawa nyumbani kwao, na pia kuonyesha kupungua kwa mwanya uliopo katika upatikanaji huduma za maji na kujisafi kati ya maeneo ya vijijini na mijini. Inasema mnamo mwaka 1990, zaidi ya asilimia 76 ya watu waishio mijini walikuwa na huduma za kujisafi, ikilinganishwa na asilimia 28 tu ya wakazi wa vijijini, lakini mwaka 2012, tofauti ilikuwa asilimia 80 ya wakazi wa mijini ikilingaishwa na asilimia 47 ya wakazi wa vijijini.