Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza lajulishwa jinsi usalama unavyokwamisha uondoaji wa 8% ya silaha za kemikali Syria

Bi. Sigrid Kaag, Mratibu wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na OPCW katika kutokomeza mpango wa silaha za kemikali Syria. (PichaUN//Mark Garten)

Baraza lajulishwa jinsi usalama unavyokwamisha uondoaji wa 8% ya silaha za kemikali Syria

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Nimejulisha baraza la usalama kuhusu maendeleo ya uondoshaji wa silaha za kemikali Syria na kubwa zaidi ni mkwamo tunaopata kumalizia asilimai Nane iliyobakia kwani maeneo ambako zinapatikana hakuna usalama.

Ni kauli ya Sigrid Kaag Mratibu wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na shirika la kimataifa la kupinga silaha za kemikali, OPCW aliyotoa alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuhutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo kwenye kikao cha faragha.

Amesema wao kama jopo wana hofu, halikadhalika wajumbe wa baraza kwani mzozo unaoendelea na uwepo wa silaha hizo vinatishia usalama.

Bi. Kaag akaulizwa ni hatua gani angependa kuona zinachukuliwa kiusalama?

(Sauti ya Kaag)

“Mamlaka zinahitaji kuingia maeneo hayo bila vikwazo vyovyote. Maeneo mengine mawili yaliyoko eneo hilo ambalo si mbali na mji mkuu Damascus, yamechuuliwa na upinzani. Barabara zenyewe zinazoelekea eneo hilo sasa hazipitiki na limeathiri uwezo wa kufika kwa watendaji wa jopo la pamoja na kwa mamlaka pia. Halikadhalika kwa uondoaji salama wa vifaa ili misafara iweze kuondoka salama.”

Bi. Kaag amesema usalama ukiimarika mamalaka zinaweza kuondosha shehena 16 na hivyo kuhitimisha jukumu hilo kwani ni operesheni inayoweza kukamilika kwa wiki moja na hivyo kukidhi kipindi kilichowekwa cha mwezi Juni.

Amesema meli za Norway na Denmark zinasubiri bandarini Lattakia kuondoa shehena hizo ilhali ile ya Marekani inasubiri kuziteketeza.