Mshikamano wa kimataifa uimarishwe kuwasaidia Wapalestina: Richard Falk

Mtaalam Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika maeneo ya Wapalestina yaliyokaliwa, Richard Falk

Mshikamano wa kimataifa uimarishwe kuwasaidia Wapalestina: Richard Falk

Mtaalam Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika maeneo ya Wapalestina yaliyokaliwa, Richard Falk, ametoa wito kwa wafanyabiashara na mashirika ya kiraia zaidi “kujiunga kwenye mshikamano wa kimataifa wa kupinga ukaaji wa Israel na utwaaji wa ardhi ya Palestina.”

Bwana Falk ambaye anaondoka kwenye wadhfa huo, ametoa wito huo kufuatia kuvunjika kwa harakati za amani za miezi tisa hivi karibuni.

Amesema Waisraeli na Wapalestina wanahitaji suluhu la haki kwa mzozo huo, kwa kuzingatia haki za binadamu, lakini awamu ya mazungumzo ya hivi karibuni ilitoa matumaini ya uongo na kuchangia kukata tamaa. Amesema mshikamano wa kimataifa unatakiwa kuimarishwa katika kupinga vitendo vya Israel.