Ban aipongeza Afrika Kusini kwa uchaguzi

8 Mei 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amewapongeza watu na serikali ya Afrika Kusini kwa kufanya uchaguzi wa ubunge na mikoa, huku kukiriopotiwa watu wengi kujitokeza kupiga kura.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Katibu Mkuu amewapa heko raia wa Afrika Kusini kwa kujitoa kwao kushiriki katika mfumo wa demokrasia ambao taifa lao limepigania kuweka, kuanzia uchaguzi wa kwanza wa rangi na makabila yote miaka 20 iliyopita.

Ban amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono Afrika Kusini katika juhudi zake za kuendeleza haki na maendeleo kwa manufaa ya wote katika jamii.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter