Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wapazia sauti watoto wa Nigeria

Najat Maalla M’jid (Picha:Maktaba)

Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wapazia sauti watoto wa Nigeria

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wamepaza sauti zao leo wakitaka kundi la lililojihami la Boko Haram kuwaachia huru mara moja watoto wa kike waliowateka nyara mwezi uliopita.

Taarifa ya pamoja ya wataalamu hao imetaka pia serikali ya Nigeria kuchukua hatua muhimu kuhakikisha watoto hao wa kike wanaachiwa wakiwa salama na wateka nyara wawajibishwe kwani uhalifu huo ni wa kuchukiza.

Miongoni mwao ni Najat Maalla M’jid mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara ya watoto, ukahaba na matumizi ya picha za ngono za watoto ambaye amelaani kitendo cha kiongozi wa Boko Haram kujitokeza hadharani kupitia mkanda wa video akikiri kuteka nyara watoto hao wa shule huko Chibok na kwamba atawauza sokoni na kuwaoza.

Maalla M’jid amesema biashara ya watoto au kuwatumikisha ni kinyume cha sheria za kimataifa za kibinadamu.

Naye Mtaalamu wa maalum wa haki za wanawake kutoka Muungano wa Afrika Soyata Maiga ameelezea utekaji huo kuwa ni kitendo cha kikatili akirejelea itifaki ya haki za wanawake ya katiba ya Muungano huo inayobainisha umri wa miaka 18 kama umri wa chini zaidi kwa ndoa na kupinga aina yoyote ya ndoa bila ridhaa ya pande zote husika.

Wataalamu wengine waliojumuika kwenye kauli hiyo ni Gulnara Shahinian, Rashida Manjoo, Ngozi Ezeilo na Frances Raday.