Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yachapisha ripoti kuhusu ukiukwaji haki za kibinadamu wakati wa mzozo wa Sudan Kusini

Mapigano nchini Sudan Kusini yamesababisha wananchi kuhama makwao na katika kusaka makazi wanakumbwa na madhila ya ukiukwaji wa haki zao. (Picha: UNMISS

UNMISS yachapisha ripoti kuhusu ukiukwaji haki za kibinadamu wakati wa mzozo wa Sudan Kusini

Ujumbe wa umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS umechapisha ripoti kuhusu ukiukwaji wa haki za kibinadamu na sheria za kimataifa nchini humo ikitaja mauaji ya kikabila, ubakaji na ukatili wa kingono, kukamatwa kiholela na kuzuiliwakamamiongoni mwa vitendo vilivyotekelezwa na pande zote kwenye mzozo huo.

Ripoti hiyo iitwayo “Mzozo nchini Sudan Kusini:Ripoti ya haki za kibinadamu inafuatia ripoti ya muda iliotolewa na UNMISS mwezi Februari na imetaja pia mashambulizi ya kupangwa nay a kulengwa kwa raia na mashambulizi katika vituo vya afya na majengo ya Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wake.

Hilde Johnson ni Mwakilishi maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa MataifaSudanKusini na Mkuu wa UNMISS.

(Sauti ya Hilde)

“ripoti hii itaonyesha mfumo wa mzozo na jinsi ukiukwaji ulivyotekelezwa Tunatoa wito kwa uchunguzi zaidi, ikimaanisha kuwa chunguzi hizo zinatapaswa kusonga mbele zaidi kuangalia kwa kina zaidi uwajibikaji kwa vitendo vya kihalifu na kubaini kwa uhakika wahalifu ni akina nani.”

UNMISS imekaribisha utafiti zaidi na wa haraka kwa njia wazi na huru na unaofikia viwango vya kimataifa na imewataka watekelezaji wa ukatili huo kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Ripoti hiyo ya UNMISS imezingatia matukio kuanzia mapigano yalipoanza tarehe 15 Disemba mwaka 2013.