Ripoti ya mwelekeo wa soko yaonyesha kushuka kwa uzalishaji wa nafaka:FAO
Ripoti ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO iliyotolewa leo imesema kuwa hali ya hewa na mizozo ya kisiasa imeathiri mwelekeo wa soko la chakula ulimwenguni huku uzalishaji wa nafaka ukitarajiwa kupungua kwa asilimia 2.4 ikilinganishwa na mwaka jana.
Hiyo ni ripoti ya kwanza kati ya mbili zinazotolewa kila mwaka ambapo kipindi kirefu cha ukame Marekani kimesababisha mavuno kidogo ya nafaka hususan mahindi lakini FAO inasema hakuna wasiwasi kuwa hali hiyo inaweza kuathiri upatikanaji wa nafaka kwenye soko.
Abdolreeza Abbassian ni mchumi mwanadamizi kutoka FAO.
Katika kipindi cha miaka migumu kama tulivyokuwa nayo karibuni, kupungua kwa kiwango hicho kungalitia wasiwasi. Hatutarajii kuwa wakati huu tutakuwa na matatizo kwa kuwa tuna akiba ya kutosha ya mchele, ngano na nafaka nyingine. Kwa hiyo kwa kuzingatia mazingira mengine kipindi cha mwaka kilichobakia na makadirio ya uzalishaji yakifikiwa, tunadhani akiba iliyopo itawezesha kutosheleza upatikanaji wa mazao na kuweka uwiano kwenye masoko.”
FAO inasema ingawa uzalishaji unaweza kupungua, bado biashara ya kimataifa inaweza kupanuka na kufikia kiwango cha ju mwaka huu wa 2014 kutokana na upatikanaji wa mazao zaidi kutoka nchi zinazouza mazao nje ya nchi bila kusahau wanunuzi kama vile Bangladesh, Indonesia na Ufilipino.
Wakati huo huo FAO imetoa ripoti yake kuhusu kipimo cha bei kinachoonyesha kuwa bei za mazo mwezi Aprili zimeshuka kwa pointi 209 kulinganisha na mwezi Machi kutokana na kushuka kwa bei za bidhaa zitokonazo na maziwa.