Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wiki ya Kampeni ya Elimu : Walemavu wapewe fursa sawa katika elimu

@UNICEF Tanzania/Giacomo Pirozzi

Wiki ya Kampeni ya Elimu : Walemavu wapewe fursa sawa katika elimu

"Haki Sawa, Fursa Sawa : Elimu na Ulemavu" ; hii ndiyo maudhui ya Wiki Ya Kampeni ya Elimu Duniani (Global Action Week) ya mwaka huu, inayoadhimishwa kwanzia Mei tarehe 4 hadi 10 kote duniani.

Katika makala ifuatayo Priscilla Lecomte anaangazia hali ilivyo Tanzania ambapo Shirika la Watoto Duniani UNICEF linahamasisha watoto wenye ulemavu ili wapate fursa za kujieleza na kujiendeleza kimasomo.