Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wengi wa wakimbizi wa Syria walioko Jordan hawapati huduma za UM

Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres akiwa kambini Azraq ilioko nchini Jordan,moja ya kambi wanokojif=hifadhi baadhi ya wakimbizi wa Syria

Wengi wa wakimbizi wa Syria walioko Jordan hawapati huduma za UM

Ni asilimia 20 tu ya wakimbizi wa Syria walioko nchini Jordan wanaoishi katika kambi, hii ni kulingana na Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini Jordan Edward Kallon, hali ambayo ameitaja kama ya kipekee.

Bwana Kallon ameelezea kwamba ni wakimbizi 600,000 waliosajiliwa na Shirika Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR lakini kati yao ni asilimia 20 tu wanaishi kambini.

Amesema asilimia 80 waliobakia wanaishi na wenyeji nchini Jordan katika mazingira hatarishi bila kupata huduma za Umoja wa Mataifa na kuongeza wanategemea zaidi huduma muhimu za kijamii zinazotolewa na serikali ya Jordan.

Kadhalika amesema kwamba kuna haja ya dharura ya kuendeleza uwekezaji Jordan ili kuhakikisha uwepo wa uwekezaji wa mahitaji ya kibinadamu na kuangalia upya mbinu zilizopo ili kuweza kukidhi mahitaji yaliyopo.

Umoja wa Mataifa unachagiza mbinu mpya za utoaji huduma za kibinadamu kuhakikisha kwamba wakimbizi walio hatarini zaidi wanafikiwa