Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la UNESCO lasisitiza umuhimu wa vyombo vya habari

Kongamano la UNESCO lasisitiza umuhimu wa vyombo vya habari

Kongamano la siku mbili liliangazia kuhusu uhuru wa vyombo vya habari limekamilika kwa kutoa wito unaoainisha namna uhuru wa kujieleza unavyochangia maendeleo.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utetezi wa vyombo vya habari UNESCO limebainisha kuwa uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari ni gurudumu muhimu linaloweza kusuma mbele shughuli za maendeleo. Pia limebainisha juu malengo ya maendeleo ya mellenia kwa kusema kuwa bila kuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari mataifa mengi yanaweza yasifikie malengo hayo.

 Zaidi ya washiriki 300 kutoka mataifa 90 walihudhuria kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu isemayo “ Uhuru wa vyombo vya habari kwa maendeleo bora”.