Ubora wa hewa unadidimia katika miji mingi duniani:WHO

Ubora wa hewa unadidimia katika miji mingi duniani:WHO

Kiwango cha ubora wa hewa ni cha chini katika nchi nyingi ulimwenguni kulingana na viwango vinavyopendekezwa na shirika la afya duniani WHO na hivyo kuweka watu katika hatari ya kuambukizwa magonjwa ya kupumua na matatizo mengine ya afya, . George Njogopa na ripoti kamili.

(Taarifa ya George)

Ripoti ya WHO kuhusiana na ubora wa hewa imezingatia miji 1600 ambayo imefanyiwa tathmini katika mataifa yapatayo 91.

Ripoti hiyo inasema kuwa kiwango cha safari hii ni kikubwa zaidi ikilinganishwa na kile kilichorekodiwa mwaka 2011 hatua ambayo inatishia usalama wa maeneo mengi.

Katika kiwango hicho imefahamika kuwa asilimia 12 ya wananchi wanaoishi kwenye miji hiyo ndiyo wanapata hewa inayolingana na viwango vilivyowekwa na WHO hatua ambayo inazidisha hali ya wasiwasi.

Ripoti hiyo imesema kuwa pamoja na changamoto zinazojitokeza bado miji inaweza kuchukua hatua za kukabiliana na hali hiyo.

Dr. Maria Neira ni Mkurugenzi wa WHO katika kitengo cha afya ya jamii na mazingira.

(Sauti ya Dr. Maria Neira)