Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asifu hatua ya nchi tano za Asia ya Kati kusaini itifaki kuhusu silaha za nyuklia.

Mlipuko wa nyuklia. (Picha-Maktaba)

Ban asifu hatua ya nchi tano za Asia ya Kati kusaini itifaki kuhusu silaha za nyuklia.

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani nchi Tano za Asia ya Kati zimetia saini itifaki ya mkataba wa kimataifa wa kuzuia uenezaji wa nyuklia kwenye ukanda huo.

Nchi hizo ni Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Turkmenistan na Uzbekistan ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha hatua hiyo akisema anaunga mkono uanzishaji wa kanda nyingine zaidi zisizo na nyuklia.

Taarifa ya Msemaji wa Umoja huo imemkariri Ban akisema kanda za namna hiyo zinaimarisha maadili ya dunia ya dhidi ya silaha za nyuklia na hivyo kusaidia udhibiti, usalama wa kikanda na uondoaji wa silaha.

Mkataba wa huo ulianza kutumika tarehe 21 Machi 2009 na ulianzisha ukanda huo wa kwanza kwenye eneo la kaskazini mwa dunia dhidi ya nyuklia