Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwenye ziara Sudan Kusini, Ban ataka mapigano yakomeshwe

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon akiwa ziarani nchini Sudan Kusini (Picha ya UM@DPKO)

Kwenye ziara Sudan Kusini, Ban ataka mapigano yakomeshwe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ambaye yuko ziarani Sudan Kusini, amerejelea wito wa kukomeshwa mapigano na kurejesha amani nchini humo ili watu wawezeshwe kurudi makwao. Alice Kariuki na taarifa kamili

(TAARIFA YA ALICE)

Bwana Ban ambaye amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa Sudan Kusini, Salvar Kiir, ameelezea kusikitishwa na hali ya wakimbizi wa ndani walioko kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa, akisema kwamba Umoja wa Mataifa unafanya kila uwezalo kuwarejesha nyumbani. Katika mkutano wao, Katibu Mkuu na Rais Kiir wamejadiliana kuhusu jinsi ya kuumaliza mzozo uliopo sasa. Baada ya mkutano huo, Bwana Ban akawaambia waandishi wa habari…

(BAN)

Akizungumza baada ya mkutano huo, Rais Kiir alisema yuko tayari kusafiri kwenda Addis Ababa ili kukutana na kuzungumza na Makamu wake wa zamani, Riek Machar ili waumalize mzozo huo

(SALVAR KIIR)