Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kubadili mtazamo wa jamii ni muhimu katika kulinda haki za mashoga:Celina Jaitly

Celina Jaitly alipozungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. (Picha:UN/Paulo Filgueiras)

Kubadili mtazamo wa jamii ni muhimu katika kulinda haki za mashoga:Celina Jaitly

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Bingwa wa kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kuwa huru na sawa  Celina Jaitly ambaye aliongoza na kushiriki uandaaji wa video  ya Bollywood ya muziki kuhusu haki za ushoga amezungumza na waandishi wa habari mjini New York na kusema kuwa haki za kundi hilo hazitalindwa kwa kubadili sheria pekee bali pia kubadili mtazamo ndani ya jamii.

Amesema huo ndio ujumbe ambao yeye na wenzake kwenye video hiyo wangependa dunia kutambua hasa pale kijana wa kiume alipotarajiwa kuleta mwenza wa maisha wa kike lakini akaleta mwenza wa kiume na hatimaye jamii yake katika ukaribisho ikamwelewa na kukubali ridhio lake.

 

(Sauti ya Celina-1)

 

“Kubadili mtazamo mara nyingi huanza na kufanya mazungumzo magumu, na kwa ule ukaribisho tumeweza kuleta mazungumzo haya kwenu kwa mbinu rahisi na njia ya  moja kwa moja iliyozoeleka ambayo ni sinema ya India au ikijulikana kama Bollywood.”

 

Celina ambaye pia alishinda taji la ulimbwende nchini India mwaka 2001 na sasa ni mama wa watoto mapacha wawili ameelezea matumaini yake.

(Sauti ya Celina-2)

Kwangu mimi nisingependa watoto wangu kukua katika mazingira ambayo watu wanatambuliwa kwa mrengo wa jinsi zao . Nataka watoto wangu wa kiume wakuzwe katika dunia  ambamo watu wanatambuliwa kwa mwenendo wao. Na natumai kuwa nitaendelea na safari hii kama nilivyoanza miaka 10 iliyopita. Na nimeendelea na safari hii licha ya vitisho kutoka pande zinazopinga, vitisho kwa watoto wangu, vitisho dhdi yangu na hata kuchafuliwa sifa yangu, na mengi ya aina hiyo.”

Kwa mujibu wa Celina nchini  India hivi sasa sheria imepitishwa kutambua watu waliobadili jinsia zao lakini bado kuna kizungumkuti kuhusu haki na mustakhbali wa mashoga na wasagaji.