Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amos atembelea Chad katika ziara ya siku mbili

Wakimbizi wa Chad

Amos atembelea Chad katika ziara ya siku mbili

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Bi. Valerie Amos leo ameanza ziara yake ya siku mbili nchini Chad ambapo anatarajiwa kuchagiza kuhusu suala la hali ya kibinadamu, hususan ukosefu wa usalama wa chakula na utapiamlo na athari za mzozo wa nchi jirani Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR nchini Chad.

Bi. Amos anatarijiwa kukutana na viongozi wa serikali na wanaharakati wa masuala ya kibinadamu kujadili mbinu za kuimarisha uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu kwa zaidi ya watu 97,000 ambao wamekimbia CAR kuelekea Chad na jinsi ya kuunga mkono mipango endelevu ya kutatua suala la utapiamlo uliokithiri na kutokuwepo na usalama wa chakula ukanda wa Sahel ilioko Chad. Katika ziara hiyo anaambatana na Robert Piper, Mratibu wa maswala ya kibinadamu ukanda wa Sahel.