Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kwa ajenda ya maendeleo baada ya 2015:UM

Chapisho katika tovuti ya UNESCO ikioanisha uhuru wa vyombo vya habari na amani.(Picha:Tovuti ya UNESCO)

Uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kwa ajenda ya maendeleo baada ya 2015:UM

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Ikiwa leo Mei Tatu ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, Umoja wa Mataifa na shirika lake la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO umesema mafanikio ya utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015 kunategemea haki ya msingi ya raia  ya kutoa maoni  yao na kujieleza.

Taarifa ya pamoja ya Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova imesema haki hizo ni muhimu ili kuwepo kwa demokrasia, uwazi, uwajibikaji na utawala wa kisheria kwani mambo hayo ni muhimu kwa utu wa binadamu, maendeleo ya kijamii, ushirikishi na maendeleo.

Wamesema hata wakati huu ambapo dunia imeelekeza jitihada zake kwenye maendeleo baada ya mwaka 2015, ni vyema kukabiliana na vitisho dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kote. Mathalani wamesema watendaji wa vyombo vya habari wanakabiliana na vikwazo vya kimfumo wanapotaka kuripoti ukweli ikiwa ni pamoja na kubinywa uhuru wao, kukamatwa na kutishiwa uhari wao na mara nyingine kuuawa.

Ban na Bokova wamesama utawala bora utakuwepo tu pale ambapo waandishi wa habari watakuwa huru kufuatilia na kuchunguza na hata kukosoa sera na vitendo mbali mbali.

Wamesema wakati vyombo vya Umoja wa Mataifa vikishirikiana na wadau wake chini ya uongozi wa UNESCO kuweka mazingira huru na salama kwa waandishi wa habari duniani kote, ni vyema siku ya leo serikali, jamii na kila mtu mmoja mmoja kutetea na kulinda uhuru huo kwani ni haki ya msingi na ina nafasi kubwa katika kufanikisha malengo ya milenia na ajenda endelevu baada ya mwaka 2015.