Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aitaka Marekani kusitisha mara moja hukumu ya kifo

Pillay aitaka Marekani kusitisha mara moja hukumu ya kifo

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay, ametoa wito kwa serikali ya Marekani isitishe mara moja utekelezaji wa hukumu ya kifo, kufuatia uchungu na mateso aliyoyapitia Bwana Clayton Lockett, ambaye aliuawa mnamo Jumanne tarehe 29 Aprili katika jimbo laOklahoma.

Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu, Ruppert Colville, amewaambia waandishi wa habari mjiniGenevakuwa mbinu iliyotumiwa kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya Bwana Lockett inaweza kutathminiwa kuwa ya kikatili na dhalilishi, kwa mujibu wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.

Clayton Lockett aliuawa kwa kutungwa dawa yenye sumu lakini dawa hiyo haikumuua papo hapo. Kifo chake ni cha pili cha aina yake kilichohusisha uchungu mwingi kutokana na sumu kutofanya kazi ipasavyo nchini Marekani kwa mwaka huu wa 2014 pekee.