Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yazungumzia hali ya uandishi wa habari Tanzania

UN Photo - Jean-Marc Ferre
@

UNESCO yazungumzia hali ya uandishi wa habari Tanzania

Nchini Tanzania hii leo kumefanyika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwani umuhimu wa vyombo vya habari katika utawala bora na maendeleo.

Maadhimisho hayo yameenda sanjari na kongamano lililofanyika mjini Arusha likiangazia pamoja na mambo mengine hali ya waandishi wa habari nchini humo kama alivyotueleza Afisa wa miradi ya habari na mawasiliano wa UNESCO Tanzania Al Amin Yusuph alipozungumza na Idhaa hii.

(Sauti Al- Amin-1)

Afisa huyo wa UNESCO akaenda mbali zaidi kuangazia mitandao ya kijamii.

(Sauti ya Al-Amin-2)

Mahojiano na Al Amin yatapatikana kwenye tovuti yetu.