Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa wa Tume za uchaguzi (NEC na ZEC) nchini Tanzania wapatiwa mafunzo kuelekea uchaguzi mkuu:UNDP

Uandikishaji wa wapiga kura Zanzibar, Novemba 2013. @UNDP

Maafisa wa Tume za uchaguzi (NEC na ZEC) nchini Tanzania wapatiwa mafunzo kuelekea uchaguzi mkuu:UNDP

Nchini Tanzania uchaguzi mkuu unafanyika mwakani ambapo tayari Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la mpango wa maendeleo, UNDP umeanza kutoa mafunzo ili kuhakikisha zoezi hilo linakidhi viwango vya kimataifa. Mafunzo hayo kwa wakufunzi ni ya wiki moja na yanatolewa na wataalamu wawili kutoka Marekani na Msumbiji wakishirikiana na wakufunzi wasaidizi wawili. Je mafunzo hayo yanahusu nini zaidi. Basi Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Godfrey Mulisa Mratibu wa mradi wa BRIDGE au uwezeshaji kwa demokrasia, utawala bora na uchaguzi katika UNDP nchini Tanzania. Kwanza anaelezea kwa nini wameamua kuendesha mafunzo hayo wakati huu.