Mkuu wa Operesheni za amani, Ladsous aanza ziara CAR

1 Mei 2014

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous, anazuru Jamhuri ya Afrika ya Kati, kuanzia leo Mei 1, ili kujadiliana na serikali ya mpito, taasisi za kimataifa, vikosi vya kulinda amani na mashirika ya kiraia kuhusu hali ya usalama na ujumbe mypa wa kulinda amani nchini humo.

Wakati wa ziara hiyo, Bwana Ladsous atakutana na Rais wa Mpito, Catherine Samba-Panza, Waziri Mkuu, rais wa Baraza la Mpito na Waziri wa Mambo ya Nje. Atakutana pia na wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wahudumu wa kibinadamu, pamoja na mwenyekiti wa kamisheni ya kimataifa ya uchunguzi kuhusu CAR.

Pamoja na mikutano hiyo, Bwana Ladsous atafanya majadiliano na wawakilishi wa mpatanishi mkuu, kikosi cha Afrika cha kulinda amani, MISCA, kikosi cha Ufaransa, Sangaris na EuFOR, wapiganaji wa zamani wa Seleka, na pia kuzuru kambi za wakimbizi wa ndani nje ya mji mkuu, Bangui.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter