Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Bi Sellassie kama mkuu wake mpya wa ukanda wa Sahel

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon

Ban amteua Bi Sellassie kama mkuu wake mpya wa ukanda wa Sahel

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-Moon amemteua Bi. Hiroute Guebre Sellassie kutoka Ethiopia kama mwakilishi wake kwa ajili ya ukanda wa Sahel na Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ukanda huo, OSES.

Bi. Guebre Sellassie anachukua nafasi ya Bwana Romano Prodi kutoka Italia ambaye amekamilisha kazi yake mwishoni mwa Januari, 2014. Ban ameeleza kufurahishwa kwake na kazi za Prodi katika kuendeleza mikakati ya Umoja wa Mataifa ukanda wa Sahel na kuleta pamoja jamii ya kimatifa katika kusaidia ukanda huo.

Bi Guebre Sellassie ana uzoefu ambao unajumuisha uratibu na usimamizi, utekelezaji na ubunifu wa sera katika masuala ya amani na usalama barani Afrika.

Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa kitengo cha siasa na Mkuu wa eneo la Goma katika Ofisi ya kuweka utulivu na amani nchini Demokrasia ya Congo kati ya mwaka 2007 na 2014.

Kabla ya kujiunga na Umoja wa Mataifa Bi. Guebre Sellassie alikuwa Mshauri wa masuala ya amani na mizozo wa OXFAM katika maeneo ya Pembe ya Afrika, Afrika Mashariki na Afrika ya kati. Kati ya mwaka1998 hadi 2004 aliwahi kushikilia wadhfa wa Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa kamati ya wanawake waafrika kwa ajili ya amani na maendeleo (AWCPD)

Bi Guebre Sellassie amabaye ni wakili alihitimu kutoka chuo cha Sorbonne Paris na amewahi kufanya kazi katika serikali ya Ethiopia