Mifumo ya kilimo ya jadi yapongezwa Uchina, Iran na Korea Kusini

1 Mei 2014

Mifumo sita ya kilimo cha jadi katika nchi za Uchina, Iran na Korea Kusini imepongezwa na Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, chini ya mkakati wake wa kutambua mifumo muhimu ya kilimo cha kiasili duniani.

Mifumo hiyo imetambuliwa kutokana na matumizi ya mbinu endelevu za ukulima.

Mfumo hiyo ni pamoja na ule wa Qanat, wa kunyunyizia maji mashamba nchini Iran, ambao umedumu kwa takriban milenia tatu, mfumo wa ‘kuta nyeusi’ zilizojengwa kwa kwa mawe yaliyotokana na volcano, zenye urefu wa kilomita elfu 22, na mfumo wa kunyunyizia mashamba ya mpunga wa Gudeuljang nchini Korea Kusini.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud