Ajenda baada ya 2015 bila mfumo wa uwajibikaji na ufuatiliaji haitakuwa na maana: Ashe

1 Mei 2014

Katika harakati za maandalizi ya agenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limefanya mjadala shirikishi kuhusu mfumo wa uwajibikaji na ufuatiliaji katika utekelezaji wa ajenda hiyo. Joshua Mmali na ripoti kamili.

(Taarifa ya Joshua)

Mjadala wa leo ni sehemu ya mijadala ya mkutano huo wa 68 wa Baraza Kuu ambapo Rais wake John Ashe katika hotuba ya ufunguzi amesema ajenda ya maendeleo itakuwa bora iwapo kila mshiriki atakuwa na mfumo wa kuwajibika na kile anachofanya kuanzia ngazi ya kimataifa, Kikanda hadi kitaifa. Amesema haipaswi kusubiri ajenda ikamilike ndio mfumo uandaliwe La hasha!

“Maendeleo ya kweli yanakuwa hatarini bila uwajibikaji bora. Serikali kila mahali zapaswa kuwajibika kwa mabunge yao, majimbo, wapiga kura na mashirika yasiyo ya kiserikali. Katika ngazi ya kitaifa, wadau wote lazima wawe an dhima ya kuhakikisha serikali zinaoanisha mipango yake ya maendeleo na ahadi zake zilizotoa kimataifa.”

Ashe hata hivyo amesema uandaaji wa mfumo huo uwe wa wazi, shirikishi na jumuishi na utumie fursa ya teknolojia za kisasa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika hotuba yake akaweka angalizo..

Tuna mifano mizuri ya mifumo ya tathmini ambazo nchi kwenye kanda zinafayiana. Tunapaswa kuiga baadhi ya uzoefu wa. Mipango kama hiyo pia inaweza kuwa katika ngazi ya kimataifa. Hata hivyo Umoja wa Mataifa pekee hauwezi kuwa jukwaa la mfumo wa uwajibikaji. Ni lazima ujumuishwe na uongozwe kupitia vyombo vya kikanda na serikali na majimbo yao.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter