Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya uhuru wa wanahabari duniani : tutunze haki hii ya msingi : Ban

Siku ya uhuru wa wanahabari duniani : tutunze haki hii ya msingi : Ban

Ban Ki-moon amesema, waandishi wanazidi kuwa hatarini katika shughuli zao, wakitekwa, kufungwa, kupigwa au kuuawa, na ni muhimu kutunza haki yao ya msingi ya kutangaza habari huru.

Ameongeza kwamba mitandao mipya ya uandishi wa habari kupitia njia ya simu, na mitanado ya kijamii kama Facebook na Twitter inaongeza kasi ya ushirikishi wa jamii na uwajibikaji wa serikali na wanasiasa.

Pamela Falk, ambaye ni mkuu wa shirika la wawakilishi wa waandishi wa habari wa Umoja wa Mataifa, anaeleza kwa nini kuongezeka kwa mitandao ya intaneti na ya jamii pia ni changamoto.

Kwa nini hali inazidi kuwa mbaya ? Kwa maoni yangu, ni kwa sababu ya Intaneti. Sisi tunasambaza habari, na kwa kuwa kuna habari nyingi zaidi zinazotoka siku hizi kuhusu makosa ya serikali, ambazo zinamulika tabia mbaya zozote, tumegeuka shabaha. Waandishi wako hatarini sasa, na ni muhimu kujali hii hali, na kuimulika.”