Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

“Lazima mtambue umuhimu wa kushirikiana”

“Lazima mtambue umuhimu wa kushirikiana”

Nchi za eneo la kaskazini na Asia ya Kati zimepaswa kutambua kuwa zinawajibu wa kukubali kushirikiana kwani bila kufanya hivyo agenda ya kuwa na maendeleo endeleo inaweza ikawa ndoto kufikiwa.

Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika kanda hiyo Dk.Shamshad Akhtar wakati wa ziara yake katika eneo la Almaty, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kutwaa wadhifa huo.

Kanda hiyo ambayo pia inahusisha eneo la Asia ya Pacific iliasisiwa kwa ajili ya kuusaidia Umoja wa Mataifa katika juhudi zake za kusukuma shughuli za maendeleo hasa kwa kuyalenga makundi maalum.

Kanda hiyo inazijumuisha nchi za Azerbaijan, Armenia, Georgia, Kazakhstan, Kyrgyzstan. Nchi nyingine ni pamoja na Shirikisho la Urusi,Tajakistan, Turkmenistan na Uzbekistan.