Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zatakiwa kuharakisha utekelezaji makubaliano ya UNFCCC

Nchi zatakiwa kuharakisha utekelezaji makubaliano ya UNFCCC

Makubaliano ya kimataifa yaliyofikiwa hivi karibuni ambayo ndiyo maamizio ya pamoja kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yanapaswa kuridhiwa na kutekelezwa kwa vitendo na nchi husika ili kufikia shabaha iliyowekwa.

Hiyo ni kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa makubaliano hayo yaliyoratibiwa na Umoja wa Mataicfa Christiana Figueres ambaye pia amesisitiza haja ya nchi wanachama kuongeza hatua kutekeleza makubaliano hayo.

Kwa mujibu wa ripoti zilizopo nchi wanachama kwenye makubaliano hayo tayari zimezindua taasisi maalumu kwenye serikali zao kwa ajili ya kuongeza msukumo juu ya utekelezaji wa makubaliano hayo lakini hata hivyo bado kuna hali ya kusua sua.

Hali hiyo inakuja wakati ikiwa imesalia mwaka mmoja kabla ya nchi hizo kukutana tena kwa ajili ya kuweka mikakati mipya ambayo itahakikisha dunia inaanza kuondokana kabisa na mienendo inayozalisha kwa wingi hewa ukaa yaani carbon.