Ban azungumza kwa simu na Salva Kiir kusisitiza amani Sudan Kusini

30 Aprili 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito akitaka kukomeshwa kwa matukio ya mauaji ya raia yanayojiri huko Sudan Kusin na kusisitiza pia hatua zinazopaswa kuchukuliwa na serikali ili kuwanusuru wananchi wanaendelea kupoteza maisha kutokana na machafuko ya kisiasa yanayoendelea.

Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais wa Sudan Kusin Salva Kiir, Ban alizungumzia pia tukio la kushambuliwa kwa kambi ya watumishi wa Umoja wa Mataifa huko Bor akisema kuwa jambo hilo halikubaliki hata kidogo.

Alitaja pia mapigano ya kikabili yaliyojiri katika eneo la Bantiu kuwa ni tukio linalopaswa kulaaniwa na wahusika wake wafikishwe kwenye mkono wa sheria.

Alisema kuwa mazungumzo yanayoendelea Addis Ababa, Ethiopia nchini ya upatanishi wa jumuiya ya kieneo ya IGAD yatazaa matunda na ni matumaini yake kwamba pande zote zinazozozana zitaheshimu makubaliano yatayofikiw

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter