Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Abdoulaye Bathily wa Senegal kuwa Mwakilishi wake Afrika ya Kati

Ban amteua Abdoulaye Bathily wa Senegal kuwa Mwakilishi wake Afrika ya Kati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, ametangaza leo kuteuliwa kwa Abdoulaye Bathily wa Senegal kuwa Mwakilishi wake Maalumu kwa ukanda wa Afrika ya Kati, na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwenye ukanda huo, UNOCA, iliyopo mjini Libreville, Gabon.

Bwana Bathily ataichukuwa nafasi ya Abou Moussa wa Chad , ambaye Ban amemshukuru kwa uongozi wake na ufanisi muhimu uliopatikana wakati wa huduma yake katika ofisi hiyo ya UNOCA.

Bathily ana uzefu mkubwa kisiasa, kidiplomasia na katika masuala ya usomi, kutokana na huduma yake katika tasisi za serikali na elimu, na pia kama mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa, ambako amekuwa akihudumu kama Naibu Mwakilishi wa katibu Mkuu katika Ujumbe wa pamoja wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA, tangu Julai 2013.