Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na National Geographic kushirikiana katika masuala ya chakula

FAO na National Geographic kushirikiana katika masuala ya chakula

Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, na Shirika la Kimarekani la National Geographic yametangaza kuanzisha kampeni ya pamoja ya kuhamasisha kuhusu chakula na masuala ya kilimo, wakati shirika la National Geographic likizindua ripoti za miezi minane kuhusu masuala ya chakula kuanzia tarehe 2 mwezi Mei. Ripoti hizo zitapatikana katika jarida lakenakwenye tovuti, NatGeoFood.com.

Uzinduzi rasmi wa ripoti hizo utaadhimishwa kwa hafla ya siku tatu kuanzia Mei 2 hadi 4 kwenye makao makuu ya National Geographic, mjiniWashington,D.C., Marekani, na kongamano kuhusu usalama wa chakula na uendelevu.

Kuanzia mwezi Mei hadi Disemba, wataalam wa FAO watatoa maelekezo na takwimu kwa uandaaji wa ripoti za National Geographic, zikiwemo ripoti za kina katika jarida la kila mwezi, na makala kwenye tovuti ya NatGeoFood.com. Mashirika hayo mawili yatahusika pia kwenye shughuli za kusaidia katika kuelimisha na kuendeleza uelewa kuhusu njaa na lishe.