Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani ghasia Iraq na apongeza kazi ya tume ya uchaguzi

Ban alaani ghasia Iraq na apongeza kazi ya tume ya uchaguzi

Uchaguzi wa wajumbe wa Iraq unatarajiwa kufanywa tarehe 30, mwezi Aprili, pamoja na uchaguzi wa halmashauri ya mkoa wa Kurdistan. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, uchaguzi huo ni hatua muhimu katika ukuaji wa demokrasia, na utachangia katika kujenga amani na utulivu nchini humo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekaribisha mafanikio ya Tume Kuu Huru ya Uchaguzi katika maandalizi ya uchaguzi kwa kufuatilia sera za kitaifa na viwango vya kimataifa.

Bwana Ban amelaani vikali mkurupuko wa ghasia na ugaidi zilizolenga viongozi wa kisiasa, wagombea na wafanyakazi wa uchaguzi, akipeleka rambirambi zake kwa familia za wahanga. Amewaomba viongozi wa kisiasa kuchangia katika kujenga mazingira ya utilivu yatakayowezesha raia wa Iraq kushiriki katika uchaguzi na kutoa maoni yao kuhusu hatma ya nchi yao.