Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Michezo yaunganisha watu wa kabila tofauti : BAN

Michezo yaunganisha watu wa kabila tofauti : BAN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, ambaye ameongoza leo majadialiano kuhusu umuhimu wa michezo katika amani na maendeleo, amemnukuu mchezaji maarufu Magic Johnson akisema : “Michezo inaleta pamoja watu wa kabila tofauti, ndiyo maana ni ya kushangilia” “We all play with different races of people when you're in sports. That's what makes sports so beautiful.”

Ameongeza kusema kwamba michezo inapunguza tofauti za kikabila, kidini, kimila au kiuchumi, na ni mbinu nafuu ya kuelimisha jamii kuhusu mambo mbalimbali, hasa kwa vijana.

Alitangaza pia kwamba Umoja wa Mataifa umesaini mkataba wa makubaliano na Kamati ya kimataifa ya olimpiki IOC, ili waendelee na ushirikiano, hasa katika maswala ya maendeleo kwa vijana.

Alichukua fursa ya kumpongeza Meb Keflezighi, mkimbizi kutoka Eritrea ambaye alishinda shindano la marathoni Boston wiki iliyopita.

Rais wa Baraza kuu, John Ashe, naye alichukua fursa kukumbusha umuhimu wa michezo.

“Kwa wengi wetu, michezo ni kitu cha muhimu katika maisha yetu, na ni muhimu sana pia kwa vijana. Ni raisi kuona faida ya michezo kwa jamii, familia, uchumi, marafiki, na nchi zote duniani. Ndiyo maana michezo na muziki ni mambo ya kimataifa, ambayo yanaweza kuungana watu kwa amani na kuchangia katika maendeleo endelevu”

Mwaka huu, Umoja wa Mataifa umeadhimisha kwa mara ya kwanza siku ya michezo duniani, tarehe 6 Aprili, ikiwa ni siku ya kwanza ya michezo ya olimpiki ya nyakati ya kisasa, mwaka 1896.