Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tupo macho kuhakikisha jaribio la silaha za nyuklia halifanyiki: CTBTO

Tupo macho kuhakikisha jaribio la silaha za nyuklia halifanyiki: CTBTO

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya miaka kumi tangu azimio namba 1540 la kupinga uenezaji wa silaha za maangamizi ya halaiki, Katibu Msimamizi wa Shirika la Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya silaha za Nyuklia, CTBTO, Lassina Zerbo, amesema shirika hilo litaendelea kuwa macho na kufuatilia kila eneo la dunia, iwe baharini, angani au chini ya ardhi ili kuhakikisha kuwa hakuna jaribio lolote la nyuklia litakalotendeka bila kutambulika.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York leo, Bwana Zerbo amesema ni vyema ulimwengu kufahamu kuwa shirika hilo la CTBTO lipo kwa ajili ya jukumu hilo. Amesema wakati huu Korea Kaskazini inapotishia kufanya jaribio jingine la silaha za nyuklia, tishio hilo lichukuliwe kama ukumbusho wa kuendelea kuwepo tatizo kubwa la kukabiliana nalo.

“Tusipobaki wima na imara kuipinga Korea Kaskazini kufanya majaribio haya ya nyuklia, tutapaswa kuwa na hofu ya kwamba sio wao pekee watakaotaka kufanya jaribio hilo. Hii ndiyo maana tunatakiwa kuikumbusha jamii ya kimataifa kuwa ulimwengu sasa umeendelea sana sasa kwa nchi zenye utaarabu kuendelea kufanya majaribio kama hayo”

Bwana Zerbo amesema kinachotakiwa kuangaziwa zaidi ni kuona kuwa uenezaji wa silaha za nyuklia umekomeshwa katika ngazi zote na kila sehemu, kwa kuhakikisha kuwa watu hawaundi silaha mpya za nyuklia.