Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wananchi wa CAR wasimulia machungu yanayowakabili.

Wananchi wa CAR wasimulia machungu yanayowakabili.

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, hali bado si shwari na kila uchao kunakuwepo na ripoti za majanga yanayozidi kukumba wananchi. Suala la mauaji kwa kuzingatia misingi ya kidini ndilo linashika nafasi kubwa ambapo tayari Umoja wa Mataifa umeunda ujumbe wake maalum nchini humo ambao utaanza kazi mwezi Septemba mwaka huu. Je wananchi wana ushuhuda upi wa yale yaliyowakumba? Ungana basi na Grace Kaneiya kwenye makala hii.