Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa Ban Ki-moon alaani shambulizi la Kosovo

Mwakilishi wa Ban Ki-moon alaani shambulizi la Kosovo

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Kosovo Farid Zarif, amelaani vikali tukio la shambulizi la mwishoni mwa juma lililenga msafara wa ujumbe wa kimataifa.

Ujumbe huo wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kwa ajili ya utawala wa kisheria kwa Kosovo ulikuwa ukisafiri kuelekea eneo la Bërnjak ndipo ulipokumbwa na shambulizi hilo.

Mjumbe huyo wa katibu mkuu katika taarifa yake ametaka wahusika wa shambulizi hilo wanasakwa na kuchukuliwa sheria. Pia amesema kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono shughuli za ujumbe huo na kuwataka kutovunjika moyo.