Kemikali za sumu eneo la kazi zatishia afya za wafanyakazi na mazingira: ILO

28 Aprili 2014

Ikiwa leo ni siku ya usalama na afya eneo la kazi, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kazi duniani, ILO Guy Rider amerejelea wito wake wa kutaka kuwepo kwa mazingira salama na ya afya kazini. Alice Kariuki na ripoti kamili.

(Taarifa ya Alice)

Mwaka huu tumetilia maanani masuala ya afya na usalama yanayohusiana na matumizi ya kemikali katika uzalishaji kwani kemikali ni sehemu kubwa ya vitu vinavyotumika kwenye uzalishaji, amesema Guy Rider kwenye ujumbe wake.

Hata hivyo amesema kemikali hizo zina madhara kwa wafanyakazi akitolea mfano saratani, ulemavu wa viungo kutokana na uwezo wa kemikali kulipuka na kusababisha moto na hata uchafuzi wa mazingira ya nchi kavu na bahari.

Mkuu huyo wa ILO amesema Ijapokuwa hatua zimechukulwa kwa kutunga sheria za kudhibiti kemikali maeneo ya kazi bado hatua zaidi zinatakiwa kwani matukio makubwa yanatokea na kuathiri afya za binadamu na mazingira

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud