Nuru yaonekana ya muarobaini wa Mbung’o aletaye magonjwa hatari kwa binadamu na wanyama.

25 Aprili 2014

Wanasayansi wamegundua mfumo wa kijenetiki wa mbungo anayefyonza damu na kusababisha magonjwa hatari kwa binadamu na wanyama hususan nchi za AFrika zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara. Priscilla Lecomte na ripoti kamili.

(Taarifa ya Priscilla)

Kwa mujibu wa FAO, uvumbuzi huo unaleta matumaini makubwa katika kutokomeza homa ya malale inayoathiri zaidi ya mifugo milioni 3 kwa mwaka, barani Afrika.

Utafiti huo uliandaliwa na FAO na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, Daktari Kostas Bourtzis ni mwana biolojia wa FAO, anaelezea umuhimu wa utafiti huo :

Kwa kufahamu vizuri mfumo wa kibiolojia na kijenitiki wa aina moja, tunaweza kubaini jinsi ya kuishambulia. Tumeweza kutambua mfumo wa kijenitiki wa aina mbalimbali za mbung’o, kwa hiyo tumeongeza ufahamu wetu wa mfumo wao wa kibaiolojia. Itatusaidia kuboresha utafiti juu ya njia za kudhibiti mbung’o na kusaidia wanasayansi kuvumbua mikakati mipya ya kutokomeza mbung’o ili tupunguze matumizi ya dawa aghali.”

Ugonjwa wa ndorobo au homa ya malale unaoathiri wanyamapori, mifugo na binadamu ungali changamoto kubwa barani Afrika kwani unashambulia mifugo mingi, unagharimu kuutibu, unasababisha vifo mara kwa mara na kupunguza mapato ya wakulima. Ni ugonjwa unaoongezeka siku hizi barani Afrika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na wakulima kukosa maeneo safi ya ufugaji.

FAO inashirikiana na nchi husika kwa kujaribu kudhibiti mbung’o kwa kuingiza madume tasa na kupuliza dawa, ingawa suluhu hiyo si endelevu kwa mazingira na afya ya mifugo.

Uvumbuzi huu wa mfumo wa kijenitki wa mbung’o utasaidia kubaini mkakati mbadala.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter