Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yalaaani shambulio la msafara wa chakula jimboni Upper Nile

UNMISS yalaaani shambulio la msafara wa chakula jimboni Upper Nile

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini UNMISS umelaani vikali shambulizi ililoliita lisilochochewa na chochote dhidi ya msafara wa chakula katika mashua iliokodishwa na UNMISS kugawa chakula cha msaada wa dharura na mafuta jimboni Upper Nile mjini Malakal.

Taarifa ya UNMISS inasema shambulio hilo limetekelezwa ziwani Nile karibu na Barbuoui ambapo msemaji wa jeshila Sudan SPLA na vikosi vya upinzani SPLAM wamekanusha kuhusika wakisema vikosi vyao haviko katika eneo hilo.

Wafanyakazi wanne katika chombo hicho na walinda amani wa UNMISS walijeruhiwa katika shambulio hio japo taarifa zinasema hakuna miongoni mwao aliyepata majeraha ya kutishia uhai.

UNMISS katika taarifa yake imerejelea wito kwa vikundi kinzani nchini Sudan Kusini kutekeleza makubaliano ya kukomesha mapigano kufuatia makubaliano waliyotia saini mjini Addis Ababa nchini Ethiopia January 23 mwak huu.