Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yakaribisha uwazi katika uchaguzi Afghanistan

UNAMA yakaribisha uwazi katika uchaguzi Afghanistan

Ofisi ya Umoja wa Mataifa Afghanistan, UNAMA, imekiri kuridhika na hatua zinazochukuliwa na mamlaka za uchaguzi nchini humo ili kuhakakisha kuwepo kwa uwazi katika zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi mkuu wa raisi.

“Inabidii tupongeze mamlaka za uchaguzi za Afghanistan kwa juhudi zao za kuhakikisha kuwepo kwa uwazi zaidi katika uchaguzi, na tuwape moyo kuchukua hatua zaidi”, alisema mwakilishi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Jan Kubis.

Akizungumza mbele ya Tume Huru ya Uchaguzi, Jan Kubis, ambaye pia ni mkuu wa UNAMA, ameongeza kwamba ni muhimu kuheshimu sheria za nchi katika zoezi la kuhesabu kura, na kuhakikisha malalamiko yote yasikike kabla ya kutangaza matokeo. Amesisitiza pia umuhimu wa kuwepo kwa uwazi, uadilifu na ukamilifu katika kazi hiyo.

Tume Huru ya Uchaguzi inatakiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi, tarehe 14, mwezi Mei.