Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya mashambulizi Somalia bado kuna fursa ya kuimarisha usalama : Balozi Kay

Licha ya mashambulizi Somalia bado kuna fursa ya kuimarisha usalama : Balozi Kay

Mwakikilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Nicholas Kay amesema licha ya taarifa za mauaji ya kiholelea nchiniSomalialakini bado kuna  fursa ya kujenga nchi na kuimarisha usalama .

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York balozi Kay ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSOM amesema ushirikaiano wa kipekee katia ya Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika umesababaisha kuimarika kwa jeshila nchi hiyo na hivyo kufanikiwa katika kusamabaratisha kundi la kigaidi la al shabaab ni na hivyo.

(SAUTI KAY)

Inatupa fursa sasa kusaidia serikali ya Somalia kuwezesha maisha bora kwa watu katika maeneo haya na ni fursa muhimu wa kulidhoofisha na na kupokonya uwezo wa al shabaab ambalo hutishia usalama wa Somalia na katika ukanda mzima

Kadhalika balozi Kay amesema licha ya juhudi hizo badoSomaliainakabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama na hivyo kuitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia katika michango ya fedha, kusaidia rasilimali kwa jeshi na kuimarisha ujumbe wa Afrika nchnihumo AMISOM.