Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam wa UM atolea wito mashauriano katika kubadilisha kamisheni ya uchaguzi: Cote D’ivore

Mtaalam wa UM atolea wito mashauriano katika kubadilisha kamisheni ya uchaguzi: Cote D’ivore

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Cote d’Ivoire, Doudou Diène, leo ametolea wito mamlaka nchini humo kupanua majadiliano katika muongozo wa kubadilisha kamisheni huru ya uchaguzi (IEC) Ili kuhakikisha nchi hiyo haitumbuki tena katika mzozo.

Bwana Diène amesema kwamba kuridhia rasimu ya muswada kuhusu kubadilisha kamisheni ni hatua muhimu katika kustawisha demokrasia nchini Côte d’Ivoire.

Hata hivyo amesema mabadiliko hayo yanapaswa kuchangia katika mchakato wa maridhiano ya nchi na kuchagiza uzinduzi wa mashauriano ya kisiasa.

Wito huu umekuja baada ya hatua ya Serikali kuridhia muswada kuhusu muundo wa IEC, mamlaka na utekelezaji kufuatia pendekezo mahususi lililotolewa na Bwana Diene katika ripoti yake kwa Kamisheni ya haki za binadamu.