Watoto huko Kachin, Myanmar wanahitaji ulinzi na amani; UNICEF

22 Aprili 2014

Mapigano ya hivi karibu kati ya jeshi la serikali nchini Myanmar pamoja na kikundi kinachotaka kujitenga kwenye jimbo la Kachin Kusini mwa nchi hiyo yamesababisha maelfu ya watu kukimbia ikiwemo watoto wapatao Elfu Moja.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Myanmar Bertrand Bainvel ambaya amesema watoto hao wamekimbia makazi yao ya muda .

Amesema kwa wengi wa watoto hao, hii ni mara ya pili au ya tatu wanalazimika kukimbia makazi yao ya muda na kwamba licha ya mapigano kutulia siku za karibuni bado hali ni tete.

Mwakilishi huyo amesema mapigano hayo pamoja na familia kukimbia makazi yao kunaweka afya za watoto hatarini zaidi ikiwemo kuzuia uwezo wao wa kupata huduma za maji safi na salama pamoja na zile za kujisafi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter