Usalama wa wakimbizi wa ndani Milioni Moja Sudan Kusini mashakani: Mtaalamu

22 Aprili 2014

Ulinzi wa wakimbizi wa ndani Milioni Moja Sudan Kusini uko hatarini kila uchao kutokana na mashambulizi ya kikabila yanayoendelea, ameonya mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wakimbizi wa ndani Chaloka Beyani.

 Beyani ambaye alitembelea Sudan Kusini Novemba mwaka jana ameelezea masikitiko yake kwa mashambulizi ya wiki iliyopita kwenye maeneo yanayofahidhi wakimbizi wa ndani ikiwemo ofisi za ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo mjini Bor.

Ametaka usalama na ulinzi wa wakimbizi wa ndani uwe kipaumbele cha hali ya juu cha Umoja wa Mataifa wakati huu ambapo mashambulio hayo ya wiki iliyopita yalisababisha vifo vya mamia ya watu na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Beyani ameshutumu vikali ghasia dhidi ya wakimbizi wa ndani Sudan Kusini akitaka pande zote kwenye mzozo unaoendelea kujiepusha na ghasia dhidi ya kundi hilo pamoja na raia huku akitaka jamii kutoka makabila yote kuepuka matumizi ya maneno ya chuki na mapigano.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter