Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulemavu usikwamishe haki ya kufanya maamuzi: Wataalam wa UM

Ulemavu usikwamishe haki ya kufanya maamuzi: Wataalam wa UM

Watu wenye ulemavu wana haki sawa kama watu wengine ya kufanya maamuzi kuhusu maisha yao, ikiwemo haki ya kufanya maamuzi magumu na kukosea, imesema kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wenye ulemavu, katika mwongozo mpya wa kutekeleza mkataba kuhusu haki za watu wenye ulemavu.

Mmoja wa wanakamati hao, Theresia Degener, amesema kuwa haki za watu wote wenye ulemavu kufanya maamuzi zinatakiwa ziheshimiwe, bila kujali ni kiwango kipi cha usaidizi wanaohitaji.

Amesema watu wenye ulemavu, wakiwemo wale wenye ulemavu wa kisaikolojia na akili ni lazima wasaidiwe kufanya maamuzi, na wala wasifanyiwe maamuzi yote, hata wakati inapodhaniwa kuwa maamuzi wanayofanyiwa ni bora kwa matakwa yao.