Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la kimataifa kuhusu mabahari na usalama wa chakula laanza The Hague

Kongamano la kimataifa kuhusu mabahari na usalama wa chakula laanza The Hague

Hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa ili kurejesha ubora wa mabahari ya dunia na kuhakikisha usalama endelevu wa chakula kwa idadi ya watu inayozidi kuongezeka duniani. Huo ndio ujumbe muhimu kwenye kongamano la kimataifa kuhusu mabahari na usalama wa chakula, ambalo limeanza leo mjini The Hague, Uholanzi.

Kongamano hilo linalomalizika mnamo Aprili 25, linawaleta pamoja mawaziri, wataalam wa sekta ya uvuvi, watu kutoka jamii za wavuvi, pamoja na wawakilishi wa mashirika ya umma, kwa minajili ya kumulika na kuongeza uwekezaji katika kukabiliana na matishio matatu kwa ubora wa mabahari, ambayo ni uvuvi wa kupindukia, uharibifu wa bayoanuai na uchafuzi.