Mbunge mwingine auawa Somalia, UM walaani vikali

22 Aprili 2014

Mbunge mwingine Abdiaziz Isaaq Mursal ameuawa nchini Somalia ikiwa ni siku moja baada ya kuuawa kwa mbunge Isaak Mohammed Rino. Kufuatia tukio hilo Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicolas Kay ameshutumu vikali tukio hilo la leo ambapo mbunge Mursal alipigwa risasi na kuuawa asubuhi ya leo na watu wenye silaha wasiojulikana.

Tayari kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab kimedai kuhusika na mashambulio hayo mawili ambapo Bwana Kay amesikitishwa na kueleza pia kuhuzunishwa na kuuawa kwa mwanahabari mmoja jana usiku.

Kay ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM amesema wanahabari wanapaswa waachwe watekeleze wajibu wao bila hofu yoyote.

Halikadhalika amesema anatiwa hofu na mashambulio hayo ya hivi karibuni lakini akisema wanaendelea na msimamo wao wa kusaidia wananchi waSomaliana wawakilishi wao wakati huu ambapo wanajitahidi kufikia matumainiyaoya kuwa na amani na mustakhbali tulivu.

Mkuu huyo wa UNSOM amesema wanaotekeleza ukatili huo hawana chochote cha kuwapatia wananchi waSomaliazaidi ya ghasia na ukosefu wa usalama na ameitaka serikali kuchunguza tukiohilona wahusika wafikishwe mbele ya sheria.

Ametuma rambirambi kwa familia za mbunge huyo pamoja na mwanahabari, halikadhalika bunge laSomaliana jamii nzima ya wanahabari nchini humo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter