Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria yaombwa isifanye uchaguzi mwezi Juni

Syria yaombwa isifanye uchaguzi mwezi Juni

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa mamlaka za Syria kutofanya uchaguzi wa urais wakati huu mgogoro unapoendelea na watu wengi wakiwa wamelazimika kuhama makwao.

Mnamo Jumatatu, serikali ya Syria ilisema kuwa uchaguzi utafanyika tarehe 3 Juni. Taifa hilo limekuwa vitani kwa kipindi cha miaka mitatu. Zaidi ya watu 100,000 wamuawa, na mamilioni yaw engine kusalia wakihitaji misaada ya kibinadamu ndani na nje ya nchi.

Stephane Dujarric ni msemaji wa Umoja wa Mataifa.

"Kufanya uchaguzi katika mazingira ya hivi sasa palipo mapigano na halaiki ya watu kuhama kutavuruga harakati za uchaguzi na kuharibu matumaini ya suluhu la kisiasa ambalo taifa hilo linahitaji kwa dharura.Uchaguzi kama huo ni kinyume na makubaliano ya mkutano wa Geneva. Hata hivyo, tutaendelea kutafuta na kutumia mwanya wowote unaoweza kuleta suluhu kwa janga la Syria.”

Kuna ripoti kuwa Spika wa Bunge ametangaza kuwa Mahakama ya Katiba itaanza kupokea maombi ya urais mnamo siku ya Jumanne.