Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wiki ya chanjo barani Afrika kuanza kesho

Wiki ya chanjo barani Afrika kuanza kesho

Utoaji chanjo ni wajibu wa pamoja, ni maudhui ya wiki ya chanjo barani Afrika itakayoanza kesho tarehe 22 hadi 27 mwezi huu ukiangazia dhima ya kila mmoja katika kufanikisha jukumu hilo adhimu.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa serikali, watumishi wa afya, wazazi, familia na jamii kwa ujumla wanapaswa kusaidia utoaji chanjo ili kuepusha magonjwa 25 yanayozuilika kwa chanjo ikiwemo surua, kifaduro, polio, vichomi, saratani ya kizazi, homa ya ini na kuhara.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki katika utoaji chanjo na Dokta Vida Makundi ni mtaalamu wa ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa nchini humo.

(Sauti ya Dkt. Vida)

Katika kipindi hicho jamii itakumbushwa siyo tu umuhimu wa kupata chanjo bali pia kuhakikisha mhusika anamaliza chanzo zote na hivyo serikali zinahamasishwa kujumuisha shughuli za utoaji chanjo na mipango ya uokoaji maisha kwa watoto, vijana, watu wazima na wazee.

Wakati wiki ya utoaji chanjo Afrika inaanza kesho, kimataifa siku wiki hiyo itaanza tarehe 24 hadi 30.