Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yasihi mikakati ya kuwapiga jeki wanawake kushiriki kwenye siasa

UNAMA yasihi mikakati ya kuwapiga jeki wanawake kushiriki kwenye siasa

Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ján Kubiš ameleezea umuhimu wa kuendelea kuwapiga jeki wanawake na kujitokeza kwenye majukwaa ya kisiasa hasa wakati huu ambapo taifa la Afghanistan lipo kwenye mchakato wa ujenzi mpya wa misingi ya kidemokrasia. Taarifa kamili na George Njogopa:

TAARIFA YA GEORGE

Akizungumza baada ya kukutana na wabunge wanawake nchini Afghanistan, mwanadiplomasia huyo aliwapongeza wanawake wa taifa hilo namna walivyoshiriki kwa wingi katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Alisema kuwa alitiwa moyo kuona idadi kubwa ya wanawake wakijitokeza kwenye uchaguzi huo kwa baadhi yao wakijitosa kwenye kuwania nafasi mbalimbali huku wengine wakichukua majukumu ya kuwa waangalizi na wengine wakiwa kwenye tume ya uchaguzi.

Bwana Kubiš, ambaye pia ni Mkuu wa Kamishna ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA, alisema kuwa mtindo huo, Afghanistan inaweza kupiga hatua kubwa.

Alibainisha kuwa kwa wanawake kushiriki kikamilifu kwenye mabaraza ya maamuzi siyo tu kwamba kutatoa sura kamili ya uwakilishi, bali pia ni hatua muhimu kusuma mbele maendeleo na ukuzaji wa uchumi