Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asifu matokeo ya mashauriano ya awali kuhusu Ukraine huko Geneva

Ban asifu matokeo ya mashauriano ya awali kuhusu Ukraine huko Geneva

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha matokeo ya awamu ya awali ya mashauriano yanayoendelea huko Geneva Uswisi kuhusu Ukraine.

Amekaririwa katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake akieleza kuwa anatiwa moyo kuwa pande zote zimeweza kuafiki masuala kadhaa muhimu na hatua za dharura za kuepusha mzozo kuendelea na wakati huo huo kusaka suluhu kwa amani.

Kila mara Katibu Mkuu amesisitiza umuhimu wa mashauriano yenye matokeo katiya pande zote husika na hiyo ndiyo njia pekee ya kupata jibu kwa njia ya amani, imesema taarifa hiyo.

Bwana Ban amerejelea kauli yake kuwa hali Ukraine bado ni tete na ni matarajio yake kuwa pande zote zitasonga mbele zikionyesha nia ya dhati ya kuendelea kushiriki kwa mashauriano tena kwa nia njema ili kutekeleza hatua zilizomo kwenye tamko la Geneva, jambo ambalo amesema litachangia suluhu la kudumu kwenye mzozo huo.