Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za kupambana na Malaria na changamoto zinazoibuka Mwanza Tanzania

Harakati za kupambana na Malaria na changamoto zinazoibuka Mwanza Tanzania

Wakati dunia inaelekea kuadhimisha siku ya Malaria duniani tarehe 25 mwezi huu, ripoti za shirika la afya duniani, WHO zinasema kuwa kiwango cha vifo vitokanavyo na Malaria duniani kimepungua kwa asilimia 48 kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kuanzia mwaka 2000 hadi 2012. Halikadhalika vifo vimepungua kwa asilimia 42 kwa makundi yote. Sababu mojawapo inayotajwa kupunguza vifo ni matumizi ya vyandarua vilivyotiwa VIUATILIFU na upuliziaji wa dawa majumbani.

Mathalani mwaka 2012 nchi 83 duniani ikiwemo 34 kutoka Afrika zilikuwa zimeridhia mapendekezo ya WHO ya kutumia vyandarua hivyo. Nchi hizo za Afrika ni pamoja naTanzaniaambayo leo ndiyo tunaangazia katika makala hii ya wiki iliyoandaliwa na Penina Kajura wa Radio washirika Afya Radio FM kutoka Mwanza. Kwenye makala hii Penina ametembelea baadhi ya familia kwenye kitongoji cha Nyanguje, wilaya ya Magu, mkoani Mwanza kujionea harakati za kupambana na Malaria na changamoto zinazoibuka.